Jeshi la polisi lawaita Dodoma wakuu wa upelelezi wa mikoa na wilaya


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, akizungumza na Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya (hawapo pichani) wakatia akifungua mafunzo ya siku mbili yanayofanyika mjini Dodoma. 

Na Demetrius Njimbwi – jeshi la Polisi


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, amewataka Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa na Wilaya, kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuzitatua changamoto zinazojitokeza katika jamii yetu hatua ambayo itasaidia kuutokomeza uhalifu na wahalifu.


Kauli hiyo ameitoa mjini Dodoma, jana wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya, mafunzo ambayo yatawajengea uwezo wa kiutendaji katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu.


Hata hivyo, IGP Mangu, amesema kuwa, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ni wazi kuwa, kasi ya utendaji kazi iongezeke ili kujenga taswira bora ya kiutendaji ya Jeshi la Polisi na kwamba suala la utoaji wa huduma bora kwa mteja ni la lazima hususan katika Nyanja ya upelelezi, alisema.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) Diwani Athumani, amesema kuwa, mafunzo haya ya siku mbili yatasaidia kuongeza kasi ya utendaji na kwamba Kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini imeandaa mafunzo haya ili kuongeza tija katika masuala ya upelezi.


Ameongeza kuwa, jumla ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya 205 wanashiriki katika mafunzo haya na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi hatua ambayo kwa pamoja itasaidia kuzuia makosa ya uhalifu na wahalifu.Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) Diwani Athumani, akitoa neno kwa Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya siku mbili inayofanyika mjini Dodoma. (Picha na Demetrius Njimbwi - Jeshi la Polisi).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo