Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi maarufu, Leo Tena cha Clouds FM, Dina Marious amejiunga rasmi na kituo cha
redio cha EFM 93.7, Dar es Salaam.
Dina ametambulishwa rasmi Jumatatu hii sambaba na uzinduzi wa kampeni ya Muziki Mnene. Akizungumza na
waandishi wa habari leo, Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa EFM, Dennis Ssebo alisema kumpata Dina Marious
kunawawezesha kuwapa wasikilizaji wao vipindi bora zaidi.
“Katika kuhakikisha tunaendelea kukupa kilicho bora zaidi kupitia vipindi vyetu mbalimbali, sanjari ya kuwa na
watangazaji mwenye ushawishi na uwezo mkubwa, leo hii tunamtambulisha kwenu mtangazaji Dina Marious
ambaye wengi uwezo wake mnaujua.
Na sasa ameungana na wenzake wenye uwezo mkubwa katika familia ya
EFM. Dina atakuwa anatangaza kuanzia saa 8, 9, lakini bado hatujapanga vizuri, lolote linaweza kutokea,” alisema
Ssebo.