Akizungumza na wafuasi wa Chadema pia UKAWA katika ofisi za Chadema mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho amesema,
“rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu,”Aidha Lowassa amesema, katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete ndipo wanyama wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania.
“Wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni Sh. 2,300. Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300. Sembe ilikuwa Sh. 250 leo ni Sh. 1,200.”
“Katika utawala wa Rais Kikwete, tembo wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia duniani kote.
“Kila aina ya mnyama ameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu. Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed (kasi), ambaye hawezi akae pembeni”