Breaking News: Deo Filikunjombe apata mpinzani Ludewa

Tume ya taifa ya Uchaguzi imelikubali pingamizi la aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Ludewa mkoani Njombe kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Msambichaka Batolomeo aliloliweka kupinga mgombea wa CCM Deo Filikunjombe (pichani) kupita bila kupingwa baada ya yeye kuenguliwa

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na tume ya taifa ya uchaguzi NEC kupitia kwa mkurugenzi wa tume hiyo Kailima Kombwey wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema baada ya kuikubali rufaa hiyo, imemrejesha mgombea huyo aendelee kugombea Ubunge wa Ludewa kupitia Chama chake cha CHADEMA

Pamoja na hayo pia tume hiyo imetolea matokeo ya rufaa mbalimbali za udiwani na ubunge zilizokatwa na wagombea mbalimbali nchi nzima


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo