Majambazi wanne waliokuwa wamejificha katika ziwa Buligi wilayani Karagwe kwa lengo la kutekeleza vitendo vya uhalifu huku wakiwa na silaha mbalimbali za kivita wameuwawa na jeshi la polisi mkoani Kagera wakati wakijiandaa kuvamia na kupora mali za wananchi katika mapambano ya kujibizana Risasi na jeshi hilo yaliyodumu kwa zaidi ya dakika tano.
Akiongea mara baada ya tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera ACP Augastine Leone Ollomi amesema jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema juu ya ujio wa majambazi hao ambao walikuwa wamejificha katika ziwa Buligi huku wakijiandaa kwenda kufanya matukio ya uhalifu katika kijiji cha Bisheshe wilayani Karagwe na kwamba majambazi hao walianza kujibizana risasi na jeshi la polisi na kufaniwa kuwaua wanne na katika tukio hilo hakuna askari yeyote aliye jeruhiwa.
Kamanda Ollomi ameongeza kwa kusema mkoa wa Kagera sasa unakabiliwa na matukio mbalimbali ikiwemo mauaji ya watu kukatwa kolomeo na matukio ya majambazi ambayo yameanza kujirudia ambapo ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kwa ujumla kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapoona viashiria vya watu wasio wawema wanaopanga njama za kufanya matukio ya kiuhalifu ili kwapamoja waze kudhibiti matukio hao yanayojitokeza mara kwa mara katika mkoa huo.
