Ni balaa....UKAWA waanza kupishana kauli

Hali ndani ya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA inatajwa kuanza kuwa tete huku suala la kumpata mgombea mmoja atakayesimama katika kinyanganyiro cha urais wa mwezi Oktoba mwaka huu likianza kuwagawa baadhi ya viongozi wa umoja huo.

Baada ya vikao vya muda mrefu vya kutafuta namna ya kumapata mgombea wa nafasi ya urais kupitia UKAWA, hatimaye Julai 11 mwaka huu kupitia mwenyekiti mwenza wa umoja huo na mwenye wa CUF taifa, Prof Ibrahimu Lipumba kuutangazia umma kuwa umoja huo utamtangaza rasmi mgombea wao Julai 14, kauli ambayo inatajwa kukivuruga chama chake cha CUF.
 
Hata hivyo duru za kisiasa za ndani zinadai kuwa kumekuwa na ushiriki tata wa CUF ndani ya UKAWA baada ya uwepo wa vuta ni kuvute juu ya chama gani kitamsimika mgombea wa urais, jambo linalohusishwa na kushindwa kuhudhuria kikao cha UKAWA kilichofanyika Julai 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
 
Licha ya wingu hilo zito, baadhi ya viongozi wa umoja huo ambao ni James Mbatia, Freeman Mbowe, na makaidi ambao ndio waliohudhulia kikao cha Julai 14 mwaka huu, wanasema wamekwisha kumpata mgombea wao na kwamba atakuwa hadharani ndani ya siku saba pekee kuanzia sasa.
 
Wakati duru nyingine za kisiasa zikisema huenda kuvuta muda wa kumtaangaza mgombea wa UKAWA ni kwa kile kinachotajwa kuwa ni kusubiri kukamilika kwa mazungumzo na moja ya vigogo wa CCM anayetajwa kuonyesha nia ya kujiunga na umoja huo, lakini CUF wanasema baraza kuu la chama hicho litakaloketi Julai 25 mwaka huu ndio litatoa taswira nzima ya mwelekeo wao ndani ya umoja huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo