Watu 35 wamefikishwa Mahakama ya KISUTU kwa kosa la kufanya mkusanyiko bila kibali na kuchoma moto kituo cha Polisi BUNJU

Watu 35 wamefikishwa mahakani leo kwa tuhuma za kuhusika na vurugu zilizotokea Ijumaa Julai 10 mwaka huu katika eneo la Bunju jijini Dar es salaa, na kusababisha kituo kidogo cha polisi Bunju kuchomwa moto.

Watu hao wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ambapo kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni ACP Camillius Wambura, watu hao wamesomewa mashitaka sita ikiwemo kufanya vurugu, kufanya mkusanyiko usio halali, kuchoma kituo cha polisi, na shitaka lingine ikiwa ni uharibifu wa mali, kutokana na magari yaliyoharibiwa siku ya tukio.

Watuhumiwa wote 35 wamekana mashitaka yanayowakabili na kurudishwa rumande hadi tarehe 27 mwezi huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena.

Siku ya Ijumaa ya Julai 8 mwezi huu, baadhi ya wakazi wa Bunju jijini Dar es salaam walifunga barabara ya Bagamoyo katika eneo la Bunju Shule wakiwemo wanafunzi wakidai kujengewa matuta baada ya mwanafunzi mmoja kugongwa gari na kufariki.
Hatua hiyo ya wakazi wa Bunju ilipelekea vurugu kubwa ambazo hatma yake ilikuwa ni kuchomwa kwa kituo cha polisi cha Bunju, tukio ambalo lililaaniwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki , ambapo jeshi la polisi limekuwa likiendelea na msako wa kuwapata waliohusika na tukio hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo