Hatimaye tume ya taifa ya uchaguzi nchini imetangaza orodha ya majimbo mapya ya uchaguzi 25 kwa Tanzania bara na majimbo mengine mapya 4 kwa upande wa visiwani Zanzibar huku ikisisitiza wanasiasa kuhakikisha wanatii kanuni na taratibu za uchaguzi mkuu kwa mwaka huu.
Orodha hiyo ndefu kwa Tanzania bara imetajwa jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu Damian Lubuva ambapo amesema tume yake ilipokea maombi kutoka karibu mikoa yote jambo lililowalazimu kufuata kanuni na sheria za ugawaji wa majimbo.
Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, baadhi ya mambo hayo mapya ni pamoja na Handen mjini, Nanyamba, Makambako, Butiama, Tarime, Tunduma, Kajimbo, Kavul, Geita mjini, Mafinga mjini, Kahama mjini, na ushetu huku kwa upande wa visiwani Zanzibar tume ikilazimika kuongeza majimbo manne tu ya uchaguzi.
Katika hatua nyingine tume hiyo imendelea na majidiliano na vyama vya siasa kuhusu kanuni mpya za uchaguzi ambapo wajumbe wa mkutano huo wameonyesha wasiwasi wao juu ya wapiga kura kupiga kura katika vituo vilivyoko ndani ya kambi za vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi zaidi ya mikoa, 21 wilaya 37, na majimbo 40 yaliwakilisha maombi ya kuomba kugawanya kwa majimbo mapya huku majimbo 10 yakiombwa kubadilishwa majina jambo ambalo tume imelitekeleza.