Picha za Mauji ya Polisi na Raia yaliyofanywa na Majambazi Usiku wa Kuamkia leo Jijini Dar

Watu saba wameuwawa kwa kupigwa risasi miongoni mwao askari polisi wanne, mtuhumiwa mmoja pamoja na raia wawili ambapo askari mmoja amejeruhiwa huku watoto wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka minne hadi mitano wakinusurika kifo katika kituo cha polisi cha Sitaki Shari baada ya watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kuvamia kituo hicho na kuiba silaha ambazo idadi yake kamili haijafahamika.

Tukio hilo linalotajwa kuwa ni la kutisha limetokea jijini Dar es Salaam katika kituo hicho ambapo tovuti hii imeshuhudia madimbwi ya damu,maganda ya risasi pamoja na visu ambapo mashuhuda wameiambia tovuti hii kuwa mmoja wa mtuhumiwa aliyeuwawa amepigwa risasi na majambazi wenzie baada ya pikipiki aliyokuwa akiitumia kushindwa kuwaka ili kuondoka katika eneo la tukio baada ya kutekeleza uhalifu huo ambapo watoto watatu waliofahamika kwa majina ya lea, Recho na Richard waliokuwa wamehifadhiwa katika kituo hicho baada ya kupotea wakinusurika.
 
Katika eneo la tukio ambalo ulinzi ulikuwa umeimarishwa vikali na askari polisi waliokuwa na silaha nzito pamoja na mabomu ya machozi wananchi walitakiwa kukaa mbali na tukio huku wakiwa wamejikusanya katika makundi kutafakari tukio hilo la aina yake ambapo baadhi yao wametoa ushauri kwa jeshi la polisi ili kukabiliana na uhalifu mpya wa kuvamia vituo vya jeshi la polisi.
 
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh Said Meck Sadiq ameelezea tukio hilo kuwa ni la aina yake na kutaka ushirikiano kutoka kwa wananchi kuwezesha kuwakamata wahalifu hao huku akiongeza kuwa nyakati za kuaminiana zimeanza kutoweka na hivyo ni vyema kuwatilia mashaka hatawale wanaoonekana kwenda katika nyumba za ibada kwa kuwa mipango ya uhalifu baadhi yake husukwa na kupangwa kwenye nyumba hizo za ibada.
 
Mkuu wa jeshi la polisi Ernest Mangu ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa jeshi hilo aliyefika katika eneo la tukio na mara baada ya kukagua na kupata maelezo ya tukio hilo ameonesha kusikitishwa na kutamka kulaani kwa nguvu zote tukio hilo huku akiongeza kuwa tukio hilo lina viashiria vya kigaidi huku akishindwa kutaja idadi ya silaha zilizoibwa kwa madai ya sababu za kiitelijensia na uchunguzi utakapokamilika taarifa rasmi itatolewa lakini akakiri kuchukuliwa kwa baadhi ya silaha.

habari kwa mujibu wa itv


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo