Raia wa kigeni 2040 wakamatwa wakiwa na vitambulisho vya kupigia kura


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Raia wa kigeni wajaribu kujipatia vitambulisho vya kupigia kura wafikia 2040 kwa mikoa ya  mikoa ya Kagera watu 708, Mara 619, Tanga 348,Kigoma 254, Rukwa 13, Kilimanjaro 12, Ruvuma 9, Geita 6, Shinyanga 7, Mtwara 3, Pwani 2, Mbeya 1, Morogoro 1 na Dar es Salaam 65. 

Hayo yamesemwa na Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari 
katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao  jijini Dar es Salaam leo.

 Aidha Irovya amesema amewakumbusha wananchi kupiga kura ni haki ya kila mwananchi wa Tanzania ana sio raia wa kigeni kujiandikisha ili apige kura kwana raia wa kigeni hana uwezo wa kupiga kura katika nchi asiko zaliwa. 


Pia Irovya amesema kuwa wananchi walio chukua paspoti za kusafiria zinapoisha muda wake ni lazima wabadilishe na kupewa nyingine wakati wowote wanapohitaji.


 Irovya ameongezea kuwa wananchi wanaotafuta paspoti za kusafiria tofauti na ofisi za uhamiaji wajue huko wanapotea paspoti zote zinapatikana katika ofisi za uhamiaji tuu na sio popote pale. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo