Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia watu 20 wakazi wa mji mdogo wa Katoro likiwemo kanisa la AGT kwa tuhuma za kuhujumu shirika la umeme Tanzania kwa kujiunganishia nishati ya umeme kwa njia za udanganyifu kinyume cha sheria za nchi.
Watuhumiwa hao wamekamatwa katika operesheni maalumu iliyohusisha maafisa usalama wa Tanesco mkoa wa Mwanza, watendaji wa Tanesco wilaya ya Geita, jeshi la polisi na waandishi wa habari ambapo mtuhumiwa aliyehusika kuwaunganishia umeme kwa njia ya wizi akiwatoza wananchi kiasi cha shilingi 35000 kwa mwezi taa moja amefanikiwa kutoroka na kumuacha mke wake akishikiliwa na jeshi la polisi kama wanavyobainisha maafisa wa Tanesco.
Baadhi ya wamiliki wa nyumba zilizokamatwa zikihujumu miundombinu ya Tanesco katika mji wa Katoro wamekanusha kuhusika na tuhuma hizo na kuwatupia lawama wapangaji wa nyumba.