Hatimaye mwanachama mpya wa Chadema Mh Edward Lowasa amechukua fomu ya kuwania nafasi ya urais huku akisisitiza kama atafanikikiwa ataunda serikali imara itakayowaletea maendeleo ya uhakika watanzania.
Majira ya mchana aliwasili makao makuu ya Chadema akisindikizwa na umati mkubwa wa wananchi, wapenzi na wanachama wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi ambapo ni wimbo mmoja tu ndio uliokuwa ukisikika.
Baada ya kuelezea vifungu vya katiba ya jamuhuri vinavyomruhusu kuwania nafasi ya urais, mwanasheria wa chama hicho Bw Tundu Lisu alisema ni kazi moja tu imesalia ya kuhakikisha wanaunda serikali ya awamu ya tano.
Miongoni mwa hoja alizojibu Mh Edward Lowasa ni pamoja na baadhi ya kauli za wasomi wanaobeza kujiunga kwakwe na upinzani ambapo amesema amefanya hivyo ilikuahakikisha watanzania wanapata mabadiliko ya kimaendeleo kwa kutumia rasilimali zilipo nchini.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe ametangaza rasmi tarehe za kuanza vikao vya chama hicho ambavyo vitamalizika kwa kumtangaza mgombea nafasi ya urais ikiwa ni pamoja na ilani itakayotumiwa Ukawa.
Katika zoezi hilo la uchukauji wa fomu lililodumu kwa saa kadhaa, barabara kadhaa za jiji la Dar es Salaam zililazimika kufungwa kupisha msafara Mh Lowasa uliokuwa ukisukumwa huku maelfu ya pikipiki yakiongoza msafara huo hadi ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Edward Lowassa akionesha fomu ya kuwania urais aliyokabidhiwa leo Makao makuu ya Chadema,Dar.
Umati wa watu waliojitokeza kumpokea Lowassa wakati akichukua fomu ya urais kupitia Chadema.
…Akisaini katika kitabu cha wageni.
Mnadhimu Mkuu kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu akitoa yake machache.
Lowassa akiwasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Dar leo.
Baada ya kuchukua fomu.
Mwenyekiti wa Chadema (kushoto) Mhe. Freeman Mbowe Mhe. Edward Lowassa (katikati) wakati wa zoezi la kuchukua fomu lililofanyika Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar .
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwa katika meza kuu ya Chadema.