NYAMA YA NG'OMBE YAADIMIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Wingu la uhaba wa nyama limetanda Dar baada ya machinjio ya Ukonga na Vingunguti kufungwa kutokana na kukithiri kwa uchafu huku machinjio nyingine za Mbagala na Tegeta nazo zikifungwa kwa sababu hiyohiyo.
Hatua ya kufungwa kwa machinjio imeonekana kuwa pigo kwa wafanyabiashara ambao ni zaidi ya 3,000 huku wengi wao wakiwa vijana.
Hatua ya kufungwa kwa machinjio hizo kumewashangaza wafanyabiashara hao ambao wamedai wanatoa ushuru ambao ni zaidi ya mamilioni kila siku lakini maeneo ya machinjio hizo bado kumekithiri uchafu.
Ni vigumu kusema tunafunga kwa muda gani ila tutafanya haraka iwezekanavyo kufuatilia suala hilo kuhakikisha kuwa usafi unafanyika”—alisema Taibu Shaibu, Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo