MBUNGE "BWEGE" ATOFAUTIANA NA WENZAKE KUHUSU KUCHOKA KWA SERIKALI YA CCM

Mbunge Suleiman Said Bungara ‘Bwege’ ametofautiana na wabunge wenzake wa upinzani wanaosema Serikali ya CCM imechoka, badala yake amesema Watanzania ndio waliochoka huku akisema kuwa wapo wabunge wanaoitetea serikali kwa kuibeba, lakini wapo wabunge wanaofanya kazi zao za kuikosoa.
Bwege alisema serikali haijachoka kama wengine wanavyosema isipokuwa waliochoka ni Watanzania wanaoibeba serikali hiyo wamechoka, wamejiandaa kuiondoa madarakani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na kuwaweka wagombea wa UKAWA madarakani.
Fungeni virago muondoke… anakuja Mbunge hapa na kusema serikali imejenga shule, Zahanati halafu baadaye wanaomba/wanalalamika miradi ya maendeleo katika majimbo yao haijatekelezwa.. Wabunge wa CCM wamechoka, wanajiaga wenyewe”—Suleiman Bwege.
Hoja ya kuchoka kwa Serikali ya CCM ilitolewa na Mbunge Tundu Lissu akiituhumu serikali hiyo kwa kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo.
Tangu siku hiyo wabunge wengi wa upinzani wanaochangia hotuba ya Waziri Mkuu wamekuwa wakitumia lugha hiyo huku Wabunge wa CCM wakijitutumua kuitetea kuwa haijachoka.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo