WAJAWAZITO WALAZIMISHWA KUFANYA USAFI KWENYE HOSPITALI YA WILAYA KONDOA

Kwa uliedhani ujauzito wa Zari ulikua feki, hapa je?Hospitali ya Wilaya Kondoa imeingia kwenye kashfa baada ya kubainika kuwa wajawazito wanaokwenda kupata matibabu wanalazimishwa kufanya usafi wodini na chooni katika Hospitali hiyo.
Taarifa kutoka Hospitalini hapo zimedai kwamba utaratibu huo umekuwepo kwa muda mrefu ambapo wanawake hao wamejikuta wakilazimika kutii na kuufuata utaratibu huo kwa muda wote.
Mimi nimekuja kujifungua kwa bahati mbaya mambo hayajawa tayari, nimeonekana nina matatizo  lakini nimefika hapa nimepangiwa zamu ya usafi, unafikiri nawezaje kukataa katika hali hii? Nalazimika kufanya ili mradi siku yangu ikifika ya kujifungua nijifungue salama, nikibisha nahofia naweza nikanyimwa huduma”—aliongea mmoja wa wagonjwa hao.
Mwandishi wa gazeti la NIPASHE alifika Hospitali hapo kwenye Wodi ya akina mama na kukuta harufu mbaya ya choo na bafu pamoja na mashuka kwenye vitanda kuwa machafu.
Ni kweli wanafanya usafi lakini sio kwa kiasi hicho wanachodai.. kwani kuna tatizo mtu kufanya usafi pale anapoishi? Maana wodini ni sawa na nyumbani kwao”—alijibu Mganga Mkuu msaidizi wa Wilaya hiyo, Abdallah Othman, na kuongeza kuwa hiyo ni sehemu ya mazoezi ya kuwaweka kwenye hali nzuri.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo