WAZIRI HUYU KUCHAPWA MAKOFI NA ASKOFU WA MBEYA


Askofu wa Kanisa Katoliki Mbeya amesema kama angekuwa na Mamlaka dhidi ya Waziri angemchapa makofi Waziri aliyeshindwa kutekeleza kauli ya kuzuia malori yanayoharibu barabara. 
 
“Yupo Waziri ambaye alisema malori makubwa yanaharibu barabara hivyo mizigo yote inatakiwa kusafirishwa kwa Reli lakini mpaka sasa hajatekeleza.. Kama ningekuwa na uwezo ningemchapa makofi”alisema Askofu Evarist Chengula.
 
Pamoja na kwamba Askofu huyo hakutaja jina la Waziri huyo lakini aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliwahi kutamka kauli kama hiyo ambapo alipoulizwa kuhusu kilichokwambisha kauli yake amesema kwamba ile haikuwa kauli yake ila ya Serikali, hivyo wa kuulizwa kwa sasa ni Waziri husika wa Wizara hiyo ambaye ni Samuel Sitta.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo