Ukosefu wa vifaa vya kujifunzia pamoja na upungufu wa mabweni ya wavulana na wasichana kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum hasa kwa wanafunzi wenye Ulbinism katika shule ya msingi Mwisenge B ni moja ya changamoto kubwa ambazo zinaikabili shule hiyo shule ambayo amesoma baba wa taifa hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere katika kata ya Mwisenge manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Mwalimu mkuu wa Shule hiyo Bw. Elias Makoro,amezungumza mara baada ya kupokea msaada wa magodoro kutoka kwa kikundi cha kijamii cha marafiki wa LowasSa kanda ya ziwa,kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum,amesema ni vyema jamii na makundi mbalimbali ya kijamii yakaendelea kutoa misaada mbalimbali ili kuweza kuwasaidia wanafunzi hao kusoma katika mazingira mazuri na kuitaka jamii kutowatenga watoto hao.
Naye Bw.Edward Matiko,akisoma taarifa wakati wa kukabidhi msaada huo mkubwa,amesema wao kama kikundi cha kijamii wameamua kutoa msaada huo wa magodoro kwa watoto wenye Albinism katika shule hiyo ili kuunga mkono matembezi ya kupinga changamoto zinazowakabili watu wenye Albinism ambayo yaliongozwa na waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa hivi karibuni pamoja kuunga mkono pia juhudi za mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr.Reginald Mengi anazofanya katika kusaidia makundi maalum katika jamii.
Awali kikundi hicho cha rafiki wa Lowasa wamefanya maandamano ya kilometa tatu kutoka musoma mjini hadi shule ya msingi Mwisenge katika kupinga vitendo vya ukatili na mauaji dhidi wa watu wenye Ulbinism.