Watu wawili wameuawa baada ya mapigano kati ya wakulima na wafugaji kuzuka katika kijiji cha mkindo wilaya ya mvomero Morogoro

Watu wawili wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya kwenye mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha chua mkindo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro baada ya wafugaji kuwavamia wakulima wakiwa mashambani.

kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa mapigano hayo yaliyogharimu vifo vya watu wawili akiwemo mkulima mmoja na mfugaji mmoja ambapo jeshi la polislisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili waliohusika na mauaji hayo.
 
BLOG HII imefika katika hospitali teule ya turiani wilaya mvomero na kujionea hali za majeruhi waliojeruhiwa katika mapigano hayo ambapo wameeleza walikuwa mashambani wakiendelea na shughuli zao za kila siku ghafla walivamiwa na kundi la wafugaji wakiwataka kuondoka maramoja mashambani ndipo wakaanza kupigwa sime na kuchomwa mikuki ambapo wametupia lawama serikali kushindwa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji huku wananchi wakiendelea kupoteza maisha.
 
Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya turiani wilayani Mvomero Dokta. Samsoni Nkolela amesema amepokea majeruhi watatu mabapo wanaendelea kupatiwa matibabu  na hali zao zinaendelea vizuri.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo