![]() |
| MBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJOMBE AKITOA SALAM ZA PASAKA KWA WAUMINI WA KANISA LA RC MAVANGA |
NA MatukioDaima Blog
MBUNGE wa Ludewa Deo Filikunjombe aipongeza tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) Kwa kusogeza mbele zoezi la upigaji kura za maoni kwa katiba inayopendekezwa na kuwa hatua iliyofikiwa katika mchakato huo ni kubwa na kumbukumbu kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete anapoondoka madakarani na urithi kwa Rais ajaye kuendeleza mchakato huo.
Filikunjombe alitoa pongezi hizo wakati akitoa salamu zake za pasaka jana kwa waumini wa madhehebu mbali mbali ya Kikristo katika wilaya ya Ludewa salam zilizoambatana na msaada wa viti ,bati ,vinada na saruji katika makanisa hayo kama moja ya utekelezaji wa ahadi zake kwa madhehebu hayo kama ambavyo walivyomuomba .
Alisema kuwa hatua ya tume ya taifa ya uchaguzi kuongeza muda katika zoezi hilo la kura za maoni kwa katiba inayopendekezwa mbali yakuwapunguzia majukumu watanzania ya kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja bado kusogezwa huko mbele kutawafanya watanzania hasa wananchi wake wa ludewa kuendelea na shughuli nyingine za uzalishaji mali.
'hakuna uharaka wa kuharakisha zoezi la upigaji kura za maoni katika katiba inayopendekezwa kwani hadi sasa hatua iliyofikiwa ni nzuri na kumbukumbu kubwa kwa rais Jakaya kikwete anapomaliza muda wake kuwa amefanya jambo hilo kubwa hadi lilipoishia na Rais ajaye ataanzia alipoishia kikwete kwa kukamilisha katiba hiyo kuliko kukimbizana kama ilivyopangwa awali kabla ya tume kusogeza mbele zoezi hilo kwa muda usiofahamika'
pia mbunge huyo aliwataka vijana kuwa wazalendo na nchi yao badala ya kukubali kutumika na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi na kuwa hatari ya vijana kutumika ni mwanzo wa nchi kuja kuingia katika machafuko kama zilivyonchi nyingine ambazo kila uchwao ni machafuko na chimbuko ni vijana wao kukosa uzalendo .
Hata hivyo alisema kuwa wakati Taifa likijiandaa kuelekea katika uchaguzi mkuu mwezi octoba mwaka huu kuna matukio makubwa ya kitaifa yanayoendelea likiwemo la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kuwa ni kipimo kwa watanzania hasa vijana kuanza kuonyesha uzalendo kwa kuwa waaminifu katika zoezi hilo badala ya kutumiwa na baadhi ya watu wanaotaka uongozi kwa kupitia njia za panya kwa maana ya kuwaandaa vikundi vya vijana kujiandikisha zaidi ya mara moja katika vituo tofauti jambo ambalo ni hatari katika nchi na kufanya hivyo ni kosa la jinai kisheria.
Huku akiwaonya vijana kuepuka kufanya udanganyifu wa kujiandikisha mara mbili katika daftari la kudumu la wapiga kura zoezi linaloendelea na kuwa hadi sasa kata ya mlangali ludewa kuna kijana mmoja ambae anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kujiandikisha zaidi ya mara moja
Filikunjombe amewataka waumini wa dini ya kikristo wilayani Ludewani mkoani Njombe kusherekea sikukuu ya kufufuka kwa Yesu kristo kwa kuendelea kuliombea Taifa kuondokanana mabalaa mbali mbali kwa mwaka huu tunapoelekea kuingia katika uchaguzi mkuu Octoba
Wakati waumini wa kikristo hapa nchini jana wakiungana na waumini wenzao ulimwenguni kusherekea kumbukumbu ya kufufuka kwa Yesu Kristo sikukuu ya pasaka makanisa wilayani Ludewa mkoani Njombe yakitumia sikukuu hiyo kuhimiza waumini wao kuepuka kujiungiza katika makundi ya kuvuruga amani ya nchi katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu .
Makanisa hayo yalitoa kauli hiyo baada ya kusoma wakara wa amani wa salam za Pasaka uliosambazwa katika makanisa yote na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe .
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Tafuteni Mwasonya wakati akitoa salam za pasaka na kumshukuru mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kwa msaada wa viti 100 vya Plastiki na kinanda kanisani hapo .
Alisema kuwa kwa upande wake hajapata kukutana ana kwa ana na mbunge Filikunjombe toka alipochangulia ila amekuwa akukutana na shughuli mbali mbali za kimaendeleo ambazo zimefanywa na mbunge huyo na kushuhudia utendaji kazi wake mkubwa katika jimbo hilo.
Hivyo alisema wana nchi wa Ludewa wana kila sababu ya kujivunia kwa kuwa na mbunge kama huyo na kama ingekuwa inaruhusiwa ndani ya kanisa kuweka picha ya kiongozi wa wananchi basi angeweka bango maalum ambalo limetolewa na mbunge Filikunjombe la kuwakumbusha wananchi wa Ludewa orodha ya wabunge waliopata kuongoza jimbo hilo hadi mwaka huu 2015 .
“ Kwa utaratibu wetu wa kanisa la Kirutheri ndani ya kanisa tunaweka picha ya Yesu Kristo pekee hata picha ya askofu wetu hatuweki ila kama ingekuwa inaruhusiwa kuweka picha za zaidi kanisani basi tungeweka picha ya orodha ya wabunge wetu lakini haturuhusiwi kufanya hivyo ……lakini orodha hiyo ya wabunge mheshimiwa Filikunjombe ametuandalia na kila mmoja atapewa na ruksa kwenda kuweka nyumbani kwake “ alisema mchungaji huyo.
Hata hivyo alisema sherehe ya kuviombea vitu hivyo vilivyotolewa na mbunge Filikunjombe na kumwombea mbunge huyo ili azidi kupata baraka zaidi ya kuongoza Ludewa wanapanga kuifanya wakati wowote baada ya sikukuu za Pasaka na kuwa siku hiyo watamwalika na mbunge ili waweze kumbariki pia.
Pia mchungaji huyo aliwataka waumini wa kanisa hilo kujiepusha na ushiriki wa vurugu zisizo na msingi katika taifa letu hasa wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu na badala yake kujikita zaidi katika maombi kwa Taifa ili nchi izidi kubarikiwa kwa amani na utulivu.
Huku Paroko ya Parokia ya Ludewa mjini Padre Cathbert Mlowe, alisema licha ya kuwa muumini katika kanisa hilo, mbunge huyo amekuwa na kasumba ya kuwasaidia watu bila kujali tofauti za imani na itikadi zao.
“Ninajua ninaweza kutafsiriwa kwa namna tofauti, lakini nitasema tu ya kwamba Filikunjombe amekuwa mfano wa viongozi wanaowakumbuka wahitaji kwa nyakati zote, na amekuwa mtu wa kurejea kwetu (Ludewa) mara kwa mara, viongozi wa aina hii ndio wanaopaswa kushikwa mkono,”
Alisema wakati ambapo taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, wapo watu watakaijitokeza na kujinasibu kwa namna tofauti, ikiwa ni pamoja na kukumbushia udugu uliopo kati yao na jamii za mahali wanapotoka ili wachaguliwe.
“Watu wanaojitokeza kwenye jumuiya zetu na kujitambulisha kwa familia na ukoo wanazotoka ili wachaguliwe, hawapaswi kupata nafasi hizo. Tujiandaye kuwachagua viongozi wanaotokana na sisi, wale wanaokumbuka na kurudi kuungana nasi katika kukabiliana na changamoto zetu kama anavyofanya huyu mwenzetu,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Anatoly Chowa, alitumia misa hiyo kujitambulisha kutokana na kuhamishiwa wilayani humo akitokea wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Chowa alisema Filikunjombe ni mbunge anayewatumikia wananchi kwa ubunifu unaokidhi mahitaji ya umma, hali iliyo tofauti na wawakilishi wengine.
Chowa aliyewahi kuwa Mbunge wa Biharamuro kwa miaka 10, alisema katika kipindi chote cha ubunge wake hakuwahi kuwasaidia wapiga kura wake kama anavyofanya Filikunjombe.
“Nimekuwa Mbunge kwa miaka 10, nimehudumu na Horace Kolimbe (maremu), Stanley Haule na Stanley Kolimba, sijawahi kuyafanya mambo ama kuwasikia wenzangu hao wakiyafanya kama anavyofanya Filikunjombe,” alisema.
Huku paroko wa RC Lupingu Chrisantus Mlelwa mbali ya kumshukuru mbunge Filikunjombe kwa salam zake za pasaka kwa waumini wa kanisa hilo bado alipongeza msaada wa kinanda kilichotolewa na mbunge huyo huku akiwataka waumini wa kanisa hilo kuzidi kuliombea Taifa na kumwombea mbunge wao huyo
