KAZI IMEANZA, ZITO KABWE NA ACT TANZANIA KUTUA SONGEA MJINI KUKINADI CHAMA CHAO

Na Andrew Chale 
Chama cha Wazalendo ACT-Tanzania kinatarajia kufanya  mkutano wake Mkoani Ruvuma, Ijumaa ya Aprili 10, katika eneo la Songea Mjini.
Kwa mujibu wa taarifa kupitia kurasa ya twitter ya chama hicho kilieleza kuwa,  viongozi wakuu wa chamaa hicho wanatarajiwa kuwa wazungumzaji wakuu huku Mwanachama  mwenye mvuto kwa vijana ambaye pia ni msanii Afande Sele kutoka Morogoro naye akitarajiwa kuwapo kwenye mkutano huo na  viongozi wa Kitaifa.
Aidha, chama hicho katika kujiimalisha,  kimeendelea kuwataka wananchi wazalendo kuwaunga mkono ikiwemo kujiunga na huduma ya kupata muito wa simu   wa chama hicho: Wimbo wa ACT Wazalendo kuwa muito wa simu yako, Kwa  mtandao wa Vodacom, Tuma sms “ACT” kwa namba 15577.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo