Kaka wa msichana huyo amesema mdogo wake ana matatizo ya akili, bibi yao amekuwa mlezi wao baada ya wazazi wao kufariki.. anasema uamuzi wa kumfungia dada yake huyo ndani ni kwa sababu ana nguvu sana na wanapomuachia anafanya fujo ikiwemo kuharibu vitu na kuwapiga watu
Waianza kumfungia ndani baada ya babu yake kufariki, babu yake ndio alikuwa anakaa nae nje wakati akiwa hai.
Mjumbe wa eneo hilo amesema ni kweli binti huyo ana matatizo na wanapomuachia alikuwa anafanya fujo, wakaamua kumfungia kwa ajili ya usalama.. Mjumbe anasema suala hilo hata ustawi wa jamii Magomeni wanajua, huyo bibi sio mchawi kama watu wanavyodai.
Baadae Polisi waliamua kumchukua bibi huyo kwa usalama kutokana na watu kutaka kumchoma moto, msichana huyo aliyekuwa amefungiwa amepelekwa Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.