Mama huyo ambae hana mahali pa kuishi amesema mume wake alimtelekeza pamoja na mtoto wake mdogo Nairobi.
“Nikaona hapana.. hii maisha ya kuteseka sitaweza kuteseka na mzee wangu yupo ikabidi nikaja hapa Nakuru.. nikamfuata nikamkuta akiwa kwa mama yake.. wanaishi pamoja na mama yake” ; — alisema mwanamke huyo aliyemfumania mume wake.
Mwanamke huyo amesema alishangaa kuona anakaribishwa na mwanamke ambae alimfahamu kama mama wa kambo wa mume wake.
“Vile alikuja akaingia tena mama akatandika vizuri kitanda wakalala kijana na mama yake.. wakalala kwa kitanda mimi nikatandikiwa chini nikalala.. asubuhi aliamka kutoka hapo vile aliamka akaenda, mimi hakunisemesha”; aliendelea kulalamika mwanamke huyo.