"Wamasai" SIMANJIRO ni noma,wapinga zoezi la kupima mipaka

Zoezi la kuweka mipaka mipya ya mkoa wa manyara na Dodoma mipaka ambayo pia inadaiwa kusababisha mgogoro  wa  muda mrefu kati ya kijiji cha KIMOTOROK na pori tengefu la mkungunero limeshindikana baada ya wakazi wa kijiji cha KIMOTOROK kulikataa  zoezi ilo kwa madai kuwa tume ya wataalam wanayofanya kazi hiyo hawakushirikishwa na mipaka inayowekwa imeingia ndani ya kijiji chao hivyo  hawapotayari kuona zoezi hilo likiendelea.

Wakizungumza baada ya  kugomea zoezi ilo na wapimaji kuondoka katika eneo ilo wakazi wa kijiji cha KIMOTOROK wamesema wameshindwa kuvumilia kuona zoezi hilo likiendelea huku wapimaji kutoka serikalini wakiendelea kupotosha kwa kuweka mipaka ndani ya kijiji chao  na wananchi wakikatazwa kushiriki na kwamba zoezi hilo linampango wa kuongeza mgogoro siyo kumaliza.
 
Mwenyekiti wa kijiji cha KIMOTOR  Elias Ormonyo amesema awali
Alipatiwa taarifa kuwa  wapima  watakuja katika eneo hilo lakini
Walipofika hakushirikishwa na cha ajabu hata yeye  mwakilishi wa
Mwananchi htakiwi kujua kinachoendelea hivyo anaunganana
Wananchi kulikataa zoezi hilo.
 
Mbunge wa simanjiro CHRISTOPHER OLE SENDEKA ameeleza masikinitiko yake kwa namna zoezi hilo ambalo lingeweza kuwa utatuzi wa mgogoro kushindikana na kuitaka serekali kuwa makini inapo tekeleza mipango yenye maslahi kwa wananchi na iwashirikishe kwakuwa wananchi wanayajui maaeneo yao kuliko mtaalam anayefika  kwa mara ya kwanza.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo