Serikali imesema tangu mwaka 2006 hadi mwaka huu matukio 56 ya uhalifu dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albinism yameripotiwa huku matukio 41 yakisababisha vifo vya watu 43 ,matukio 13 yakisababisha watu 13 kujeruhiwa na mengine mawili yakisababisha watu wawili kupotea.
Naibu Waziri wa mambo ya ndani Pereirra Silima amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali yanayohusiana na madhila yanayowakumba watu wenye ulemavu wa ngozi hapa nchini.
Amesema bado Serikali inawasaka watu ambao wanatuhumiwa kujihusisha na matukio ya hivi karibuni yakiwemo kuwatafuta watu 2 wenye ulemavu wa ngozi waliopotea.
Kwa sasa Taifa la Tanzania lipo katika sintofahamu kutokana na madhila yanayoendelea dhidi ya watu wenye ulemavu huo wa Ngozi albinism hali inayowafanya waishi maisha ya mashaka.