UPDATES: TAARIFA YA NYONGEZA/UFAFANUZI YA TUKIO LA KULA NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA AKIWA HOSPITALI


jana tarehe 30/03/2015 waandishi wa habari walifika kituo Kikuu

cha Polisi wakitaka kujua uhalali wa silaha iliyokamatwa tarehe 

29/03/2015. Silaha hiyo ni Bastola aina ya BERRETA yenye 

namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu. Pia zilikamatwa risasi 17 za 

Short Gun. 



Ufafanuzu ni kama ifuatavyo: 


Uchunguzi wa kina na wa kitaalam sasa umethibitisha kwamba 

silaha hiyo inamilikiwa kihalali na Askofu Josephat Gwajima. 

Kuhusu risasi 17 za Short Gun ni kwamba Askofu Gwajima 

anamiliki Bunduki aina ya Short Gun yenye namba 102837 

ambayo inatumia risasi za aina ya hizo zilizokamatwa. 





Kuhusu watu 15 wanaotuhumiwa kujaribu kumtorosha Askofu 

Josephat Gwajima bado uchunguzi unaendelea. Aidha watu hao 

pia wanahojiwa kuhusu suala la kukutwa na silaha na risasi 

zilizotajwa hapo juu wakati wao sio wamiliki halali za silaha hiyo 

na risasi hizo na idadi iliyotajwa kwa mujibu wa sheria.



Baada ya uchunguzi wa suala hilo jalada la kesi litapelekwa kwa 

mwanasheria wa Serikali kabla hawajafikishwa mahakamani ili 

sheria ichukue mkondo wake.



KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,

S. H. KOVA,

DAR ES SALAAM.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo