Wakala wa barabara Tanroad mkoa wa Morogoro wamelazimika kutumia
tingatinga kuvunja vibanda na kuta za mabaa yaliojengwa ndani ya
maeneo ya hifadhi ya barabara katika barabara kuu ya Morogoro Dodoma.
blog hii imehsuhudia baadhi ya wananchi wakibomoa na kuhamisha mali zao
baada ya tingatinga kuanza zoezi la ubomoaji ambapo meneja wa Tanroad
mkoa wa Morogoro Eng Doroth Mtenga amesema taratibu zote zimefuatwa
ikiwa ni pamoja na kuwapa taarifa wananchi juu ya zoezi la uvunjaji
lakini walikaidi amri hiyo ambapo amesema zoezi hilo ni endelevu na
hawatalipwa fidia yoyote kuwataka wananchi wengine waliojenga ndani ya
mita 22.5 katika hifadhi ya barabara kuu ikiwemo ya barabara ya
Morogoro Dar es Salaam na Morogoro Iringa kuvunja kwahiari ili kupisha
shughuli za maendelezo ya barabara pamoja na usalama wa wananchi
wenyewe.
Kwa upande wao wananchi waliovunjiwa vibanda na kuta wakiwemo
wamiliki wa mabar wakizungumzia uvunjaji huo wamekiri kuwa walipewa
taarifa za uvunjaji na wengine wakiiri kujenga katika hifadhi ya barabara
ambapo baadhi ya wakazi wa mkoa wa morogoro wamepongeza hatua
iliochukuliwa na wakala wa barabara Tanroad kutokana na baadhi ya
wafanyabiashara kutaka kupata faidha bila kujali usalama wa wananchi
