Saa zinahesabika toka Tanzania na familia ya bongofleva ipokee taarifa za msiba wa Abdul Bonge Mwanzilishi wa kundi maarufu la Bongofleva Tiptop Connection lenye wanachama kama Tunda Man, Madee, Dogo Janja na wengine waliopita kama Keisha, Cassim Mnganga na MB Dogg.
Jioni ya March 28 2015 ndio taarifa zilianza kusambaa lakini chanzo cha kifo cha ghafla cha Abdul hakikuwa kimesemwa lakini mdogo wake ambae ni Babu Tale ameongea na kusema >>> ‘Kuna mshkaji wetu mmoja alikua anagombana na mke wake jirani yetu, wakamfata hapa Abdul aende… mara ya kwanza na ya pili akakataa, mara ya tatu akasema ngoja aende’
Taarifa kutoka msibani March 29 2015 zinasema Abdul atasafirishwa kwenda kuzikwa Morogoro baada ya mwili kuzuiliwa leo mpaka uchunguzi ukamilike, kwa sasa Watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa bongofleva wako Tiptop Manzese kwenye kutoa pole, mwili unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Morogoro.
Naambiwa maziko yatafanyika kijiji cha Mkuyuni Morogoro, kwa asiyepajua Mkuyuni ni njia ya kwenda Matombo. #RIP #AbduBonge
CREDITS:MILLARDAYO.COM