SERIKALI YATANGAZA HUVIFUNGIA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA, KISA ULAFI WA WAMILIKI

Serikali imetangaza kuvifunga baadhi ya vituo vya kulelea yatima kwenye Mikoa mbalimbali Tanzania kutokana na kukiuka Sheria uanzishwaji wake pamoja na vingine kubainika kuanzishwa ili kunufaisha wamiliki.
Mbali na hatua hiyo Serikali imesema inaendelea na uchunguzi ili kubaini vituo vingine ambavyo ni vya aina hiyo.
Kaimu Kamishna wa Haki za Mtoto, Steven Gumbo amesema kuwa uamuzi wa kuvifunga vituo hivyo umekuja baada ya kufanyika utafiti kwa Mikoa 25 na kubaini kuwa vituo hivyo viko zaidi ya 300 huku vingi vikiendeshwa bila leseni.
Akizungumzia kuhusu uamuzi huo, Ofisa wa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Hai, Helga Saimon amesema Wilaya hiyo ilikuwa na vituo zaidi ya 22 lakini ni vituo 7 tu ambavyo vilikuwa vikiendeshwa kwa kukidhi vigezo.
Tulibaini mambo ya ajabu, kituo kimoja tulikuta mmiliki ni shoga na alikuwa akiwafanyisha watoto ushoga”—alisema Helga Saimon.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo