Kuna tamaduni nyingine hutumia nyama ya mbwa kama kitoweo na wakati mwingine huamini ina faida kubwa mwilini tofauti na nyama ambazo zimezoeleka kuliwa na binadamu.
Hii imetokea huko India baada ya mwanamke mmoja kumlazimisha mtoto wake kula nyama ya panya kama kitoweo cha asubuhi kwa madai watamsaidia kumpatia nguvu.
Awali mtoto huyo alidhani hawakuwa panya bali sungura lakini alipokuja kuujua ukweli alikataa kula lakini mama yake aliendelea kumlazimisha.
Alimsisitiza kuwa panya mmoja ana uwezo wa kumpatia vitamini mwilini sawa na kula kuku watatu.