Serikali yawasilisha bungeni muswada wa sheria ya baraza la vijana ya 2015 utakao boresha maisha ya vijana

Serikali imewasilisha bungeni muswada wa sheria ya baraza la vijana Tanzania wa mwaka 2015 ambao pamoja na mambo  mengine umelenga kuboresha maisha ya vijana huku vijembe vikizuka kati ya Spika wa Bunge Mhe.Anna Makinda na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi.
Akiwasilisha muswada huo,waziri wa habari,utamaduni na michezo Dr.Fennella Mkangara amesema kupitia baraza hilo kero zinazowakabili vijana hapa nchini zitatatuliwa huku vijana hao wakiwa na chanzo rasmi cha kutetea haki zao.
 
Naye mwenyekiti wa kamati ya kudumu  ya maendeleo ya jamii Said Mtanda na Msemaji wa kambi ya upinzani katika Wizara ya habari,utamaduni na michezo Joseph Mbilinyi  wamekinzana kuhusiana na jinsi ambavyo baraza hilo litakavyosaidia vijana hapa nchini sambamba na hofu ya Serikali dhidi ya baraza hilo.
 
Baadhi ya wabunge waliochangia muswada huo wamesema ni bora mapungufu yaliyopo yakatatuliwa ili kuufanya uwe na tija kwa taifa.
 
Katika hatua nyingine Spika wa bunge Mhe.Anna Makinda pamoja na mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi wamejikuta wakilumbana wakati Mhe.Mbilinyi alipoomba muongozo wa spika kuhusiana na maduka kufungwa katika miji mikubwa hapa nchini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo