PICHA: Watu watano wamejeruhiwa vibaya baada ya kuangukiwa na kifusi katika eneo la barabara ya nyerere jijini Mwanza

Watu watano wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya rufaa Bugando, baada ya kuangukiwa na kifusi cha ukuta wa jengo la biashara la Ghorofa saba linalojengwa katika eneo la barabara ya nyerere jijini Mwanza, huku askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji,polisi na mgambo wa jiji wakiendelea kumtafuta mtu mmoja anayedaiwa kufukiwa ndani ya shimo lenye urefu wa zaidi ya mita tatu.

Hawa ni mamia ya wakazi wa jiji la mwanza wakishuhudia kuanguka kwa ukuta wa jengo la biashara lililopo kitalu namba 6, block ‘U’mtaa wa Nyerere, linalojengwa na mkandarasi kampuni ya HYSCON ENGINEERING LTD YA Mwanza.
Muda mfupi baada ya ukuta huo kuanguka na kusababisha majeruhi, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya nyamagana,ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Baraka Konisaga imewasili katika eneo hilo na kutoa agizo kwa uongozi wa halmashauri ya jiji la Mwanza.
Kisha  Tukapiga shoto, kulia hadi katika hospitali ya rufaa Bugando ili kuona hali za majeruhi waliolazwa katika idara ya dharura zinavyoendelea, ambapo Daktari wa zamu katika idara hiyo Dk. Ernest Elisenguo amesema majeruhi wawili, Benson Daud na Ramadhan Mkumba hali zao haziridhishi.
IMG-20150330-WA0018
IMG-20150330-WA0020
IMG-20150330-WA0027
IMG-20150330-WA0028
IMG-20150330-WA0032
IMG-20150330-WA0035
IMG-20150330-WA0037
IMG-20150330-WA0039Taarifa iliyoripotiwa na ITV muda mfupi uliopita imesema majeruhi wawili kati ya watano hali zao sio nzuri.picha kwa mujibu wa millardayo.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo