MTOTO WA MIAKA 13 APIGA KAKA YAKE RISASI

Hii ya leo inahusu tukio lililotokea huko Florida Marekani, ambapo mtoto mwenye umri wa miaka 13, amemshambulia kaka yake mwenye umri wa miaka 16 pamoja na mdogo wake mwenye umri wa miaka 6, kwa kuwapiga na risasi halafu akajipiga mwenyewe.
Polisi wamesema watoto hao walikuwa peke yao nyumbani kwao wakati mama yao akiwa kazini wakaanza kugombania chakula, mtoto huyo akachukua bastola na kuanza kuwashambulia wenzake, kaka yake alipiga simu Polisi  ambao walifika eneo la tukio na kumkimbiza Hospitali lakini mtoto aliyewapiga risasi pamoja na mdogo wake walikutwa wameshafariki.
29906170001_4135510305001_video-still-for-video-4135458285001
Polisi wakiwa eneo la tukio
Polisi wanafanya uchunguzi kujua jinsi mtoto huyo alivyoweza kupata silaha hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo