Mwandishi
maarufu wa kituo cha Televisheni kutoka Afrika Kusini amevamiwa na
vibaka hadharani wakati alipokuwa akijiandaa kurusha habari Live kutoka
Hospitali millpark
Katika mkanda wa video umewaonyesha vijana wawili wakimvamia Vuyo Mvoko akiwa mbele ya kamera za Televisheni ya Taifa ya South Africa (SABC)
ambapo alikuwa jirani na hospitali ya Milpark, Johannesburg akiripoti
kuwasili kwa rais wa Zambia ambaye alikuwa akifikishwa hospitali hapo
kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Hata hivyo mwandishi huyo alisema kuwa
mmoja wa wezi hao alitishia kumpiga bunduki alipokataa kumpa simu yake,
hawakuonekana kutojali kamera zilizokuwa mbele yao.
Muda mfupi baadaye Mvoko
ambaye ni mhariri wa kituo hicho cha habari alituma ujumbe katika
ukurasa wake Twitter akisema kuwa yuko salama na kutuma
video mtandaoni inayoonyesha vijana hao wakimvamia.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wezi hao waliiba laptop na simu, Polisi wamesema maafisa wanachunguza tukio hilo.