Wanananchi wa kijiji cha msisi wilaya ya Bahi mkoani Dodoma,
wameuzuia kwa muda, msafara wa katibu mkuu wa CCM taifa ndugu
Abdulrahman Kinana, wakilalamikia vyumba vitatu vya shule iliyoezuliwa
paa na upepo tangu mwaka 2011 kutokukarabatiwa, hali iliyo wapelekea
wanafunzi wa shule hiyo kusomea chini ya mti na kwenye mahema kwa miaka
minne mfululizo.
Wananchi hao wanalalamikia uongozi wa halamshauri ya wilaya ya Bahi
na mkoa wa Dodoma kwa kushindwa kukarabati shule hiyo kwa mika minne
mfululizo licha ya viongozi wa juu wa mkoa na wilaya na mbunge wao kuwa
na taarifa, ambapo wanasema kuwa tangu mwaka 2011, watoto wao wamekuwa
wakishindwa kuhudhuria shule vyema na nyakati za mvua na jua kali
wanafunzi hupewa likizo ya muda hivyo kuathiri hali ya elimu kwa watoto
wao.
Uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, umejukuta
na kigugumizi mbele ya umati wa wananchi ulitaka kujua ni lini shule
hiyo itakarabatiwa, ambapo katibu mkuu wa CCM taifa ndugu Abdularahman
Kinana amewaagiza watendaji kushughulikia tatizo hilo kwani ni la muda
mrefu ambapo ameshangazwa na uongozi wa wilaya kukaa kimya kama tatizo
hilo hawalioni.
Akiendelea na ziara yake katika mkoa wa Dodoma katibu mkuu huyo wa
CCM taifa, alishiriki kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendelo ya
wananchi, kushiriki kwenye kilimo, utandazaji wa mabomba ya maji safi,
kuhutubia wananchi, ambapo wamewaomba wananchi wa Bahi kutunza Mazingira
kwa kuto kata miti ili kuhufadhi mazingira.