Kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Manyara imetembelea katika migodi
iliyoteketea kwa moto katika machimbo ya Tanzanite Mirereani Simanjiro
huku mkuu wa mkoa huo Joel Bendera akiwaagiza wataalam wa Tanesco idara
ya madini na jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka kugundua
chanzo cha moto huo ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakao
bainika.
Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa aliongozana na wataalam wa Tanesco
idara ya madini na vyombo vya ulinzi na usalama ambapo kabla ya
kuzungumza na wananchi alitoa nafasi kwa waathirika kutoa madukuduku yao
nawo waliendelea kulalamikia uzembe uliyofanyika katika tukio ilo na
kuendelea kusisitiza kuwa kuna hujuma katika tukio ilo na wengine
wakilalamikia njaa na mazingira magumu ya kulala.
Akitoa maelezo ya awali mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mahamud Kambona
ameeleza namna tukio ilo lilivyo waathiri wachimbaji wadogo na hatua za
awali walizochukua.
Ukafika wakati wa mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera kutoa
pole kwa niaba ya serikali na kuviagiza vyombo vinavyo husika kufanya
uchunguzi wa kina kwa haraka ili kujuwa kama ilikuwa ni ajali ya kawaida
au ni hujuma huku mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Christopher
Fuime akitoa angalizo kwa wachimbaji wadogo kuhusu uhifadhi na matumizi
ya mulipuko.