Jinsi zawadi zilivyozua Hekaheka Kigogo Dar.. Sherehe yafanyika kurudisha zawadi

bmx-bike-sunday-bikes-primer-16-21Story iliyosikika kwenye Hekaheka ya JANA inahusu mama ambaye aliwahi kumpa zawadi rafiki yake baiskeli kwenye sherehe ya mtoto wake pamoja na vitu mbalimbali, baadae kukaanza story kwamba aliyetoa zawadi hizo alikuwa akimtangazia vibaya kwa watu.
Mama huyo aliyetoa zawadi alikuwa akisambaza taarifa kwamba alitoa zawadi kitambaa cha sare ya nguo ya shule kwenye sherehe ya mtoto wa mama huyo mwingine, lakini mama wa mtoto huyo hakumtuza vitu vya thamani kama ambavyo yeye alitoa.
Mama huyo amesema rafiki yake alimtaarifu kuhusu sherehe ya mwanae lakini akamwambia hana kitu kwa muda huo kwa ajili ya kuandaa zawadi, akampelekea zawadi ya kitambaa lakini baadae akapata taarifa kwamba anatangazwa kwamba hana fadhila.
Alipopata taarifa za maneno hayo aliamua kununua vitu alivyopewa zawadi hizo na kukodi ngoma ya mdundiko kwa ajili ya kwenda kumrudishia, alipofika nyumbani kwake mwanamke huyo hakutoka ndani, akaamua kukabidhi vitu hivyo kwa majirani ili akitoka wampatie.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza Hekaheka yote…


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo