Jeshi
la polisi mkoani Simiyu limewaonya wafanyabiashara na wananchi kwa
ujumla kuuacha kuamini kuwa viungo vya walemavu wa ngozi Alibino
vinaleta utajili bali wafanye kazi na biashara zao kwa kufuata taratibu
sheria za nchi.
Onyo hilo limetolewa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Simyu,
kamshina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi, Charles Mkumbo wakati
alipokuwa akiwahutubia wananchi wa vijiji vya Jija na Shishiyu vilivyoko
katika kata ya jija tarafa ya Sengerema wilayani maswa ambavyo ndivyo
vinaongoza katika ukataji wa mapangana mauaji ya vikongwe ikiwa ni
sehemu ya ziara yake ya wilaya hiyo ya kuaelimu juu ya mauaji ya
walemavu wa ngozi.
Aidha kamanda Mkumbo amesema mauaji mengi Alibino na vikongwe
yamekuwa yakipangwa na familia kwa kukaa vikao na kupanga mikakati jambo
alilosema ni kosa kisheria na kuwata waache mara moja kwani
watakabainika mkono sheria utawashughurikia.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wasema kuwa kinachowavunja moyo
wa kutoa siri za wauaji wa Alibino na wakataji mapanga vikongwe ni
baadhi ya askari polisi wanaopeleleza kesi hizo wamekuwa siyo wasiri
pindi wapewapo taarifa za siri dhidi ya wauaji hao huzivujisha kwa
watuhumiwa jambo walilosema linawakosesha imani na jeshi hilo.
Wakati huohuo jeshi hilo limeanza msako wa kuwasaka na kuwakamata
waganga wa jadi wanaopiga ramuli chonganishi baada ya kubainika kuwa
ndio wanachochea kuongezeka kwa vitendo vya mauaji ya walemavu wa ngozi
Albino na vikongwe.