skip to main |
skip to sidebar
RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU DAR
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dr. Binilith
Satano Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati
wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini
Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR.jpg)
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri na Manaibu Waziri waliokuwa
wakiapishwa Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 wakati alipokuwa akiwasili
katika hafla hiyo. Picha na OMR
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha
Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30,
2014. Picha na OMR
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha George Boniface
Tuguluvala Simbachawene, kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, wakati wa hafla fupi ya
kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,
leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Saning’o Telele,
kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa hafla fupi ya
kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo
Jan 30, 2014. Picha na OMR
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakia katika picha ya pamoja na Waziri na
Manaibu Waziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam,
leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri
wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi
iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa
ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,
Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri,
iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi