Jeshi, la polisi Arusha latoa onyo kwa polisi jamii kuacha tabia ya kutumia kivuli cha jeshi hilo kutenda maovu

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limetoa onyo kali kwa askari wa polisi jamii kuacha tabia ya kutumia kivuri cha jeshi ilo kutenda maovu kwa kuonea raia na pengine kunyang’anya mali za watu kwakuwa lengo la kuanzishwa kwake ni kusaidia jamii na siyo kuikandamiza.

Viongozi wakuu wa jeshi la polisi wilaya na mkoa wa Arusha wametoa kauli hiyo walipokutana na vijana wa polisi jamii katika kata ya moshono na kulazimika kutoa kauli hiyo kufuatia malamamiko ya baadhi ya watu kufanyiwa matendo mabaya na vijana wa polisi jamii ambao lengo la kuanzashwa kwake ni kuimalisha ulinzi na si vinginevyo na kwamba jeshi ilo halitavumilia mtu yoyote atakaye bainika kwenda kinyume na matakwa hayo.

Kwa upande wao vijana hao wanashiriki katika ulinzi shirikishi wamesema wanakabiliwa na hali ngumu ya vitendea kazi kama usafiri na kwamba wanapokuwa katika ulinzi nyakati za usiku wanakutana na matisho mengi kutoka kwa waharifu wenye silaa kali wamelitaka jeshi ilo kuongeza idadi ya askari wanaoshirikiana nawo pamoja na silaa.

Diwani wa kata ya moshono Paulo Mattysen amesema kwa kushirikia na viongozi wa pilisi hakuna kitakacho haribika kwani anaimani kuwa mapungufu yatafanyiwa kazi kuimalisha ulinzi shirikishi kwakuwa eneo ilo linamatendo mengi ya uharifu hivyo polisi jamii wana nafasi kubwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo