Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakimjulia hali Meja Peter
Lyamuya aliyelazwa katika hospitali kuu ya jeshi Lugalo jijini Dar es
Salaam akiuguza jeraha la mguu alilopata baada ya ndege ya kivita
aliyokuwa akiiendesha kuanguka na kulipuka wiki iliyopita.
Askari huyo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) alinusurika kifo baada ya kufanikiwa kujiokoa katika ajali hiyo iliyosababishwa na ndege mnyama kuingia kwenye injini na kusababisha hitilafu iliyopelekea kushika moto, kuanguka na kulipuka.Ndege hiyo ilikuwa katika mazoezi ya kawaida kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza.(picha na Freddy Maro).