Abiria anagoma kutoka ndani ya chumba cha Rubani kwenye ndege…!!!!

cockpit_cover
Kwenye story ambazo zinahusu matukio ya kushtua na kushangaza kwa upande mwingine ni hii ya jamaa ambaye aligoma kushuka kwenye ndege baada ya ndege hiyo kutua, story ikazidi uukubwa baada ya jamaa huyo kwenda kujificha katika chumba  ambacho wanakaa marubani.

Maofisa wa usalama wa Uwanja wa ndege New York walitumia nguvu kumtoa jamaa huyo ambaye anaishi New Jersey , muda wote aligoma kushuka kwenye ndege akidai kwamba kuna kundi la watu walikuwa wanataka kumdhuru.
.
Ndege ya Shirika la ndege la Jetblue Airways ambayo jamaa alikuwa amejificha ndani.

Baada ya kutolewa alipelekwa Hospitali ya Jamaica ili kumcheki kama ana tatizo lolote la akili huku wakimfungulia mashitaka kwa kufanya kosa hilo.

Ndege hiyo ilitua New York ikitokea Jamhuri ya Dominica.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo