Serikali
imeshauriwa kuwawajibisha na kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi
wa kina, watumishi wake wote, wanaotuhumiwa kuhusika na uchotwaji wa
fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambao wana hojiwa na
kuchunguzwa, huku tayari chama cha mapinduzi kupitia kamati kuu
kimewawajibisha viongozi waliohusika katika sakata hilo.
Akihutubia mamia ya wakazi wa Dodoma mjini na viunga vyake katibu
mkuu wa chama cha mapinduzi CCM taifa ndugu Abdulrahmn Kinana,
amemshauri katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue kuwawajibisha
ikiwemo kuwasimaisha kazi watumishi wa serikali waliotajwa kuhusika na
akaunti ya Tegeta Escrow.
Aidha ndugu Kinana amekemea tabia ya viongozi wa serikali
wanaoteuliwa kufanya sherehe ya kujipongeza, bila ya kutambua majukumu
na mzigo unao wakibili, huku akisema kuwa, wananchi Wamekuwa wakikerwa na tabia ya wizi wa mali za umma unaofanywa na
watumishi wa umma bila ya kuwajibishwa kwa wanaotuhumiwa, na badala yake
mwizi kupewa muda wa kujitetea huku kundi linguine likiibuka na kuanza
kuwatetea wezi wa mali za umma na wasio na uadilifu.
Katibu mkuu huyo wa CCM taifa pia ameitaka serikali kuacha tabia ya
matumizi mabaya ya fedha za umma kwa idara, taasisi na wizara kutumia
kiasi kikubwa cha fedha kwaajili ya kununua mafulana na kofia na
kuwaagiza viongozi na wanachama wa CCM kutokaa kimya pale wanapoona
serikali ikifanya vibaya na inapofanya vizuri waisifu, kwani mwisho
lawama zote hugeukia chama cha mapinduzi kilichoomba kura kwa wananchi.
Kabla ya kuwahutubiwa wananchi katibu mkuu wa CCM taifa ndugu
Abdulrahman Kinana akiwa ameongozana na katibu wa NEC itikadi na uenezi
wa CCM taifa ndugu Nape Nnauye warishiriki kukagua na kuhimiza
ukamiliswahi wa miradi ya maendelo ya wananchi na kuongea na wananchi
waliojitokeza kumlaki kila kijiji alipokuwa msafara wake.