Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amesema anajivunia kuona anamaliza muda wake
akiwa amefanikisha kujenga msingi imara ya kuwawezesha na kuwapa nafasi
wanawake katika ngazi za uongozi na hivyo kuwata viongozi wajao
waendelee kuwapa fursa wanawake katika kuendeleza taifa.
Rais Kikwete ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati wa maadhimisho
ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika kitaifa katika uwanja wa
jamhuri mjini Morogoro ambapo amesema anamaliza muda wake akiwa na amani
kwa kuwa serikali imepiga hatua katika kuwaendeleza wanawake na kwa
kutambua mchango wao katika ngazi ya kupunguza umasikini na kuendeleza
taifa.
Aidha rais Kikwete amesema tunapofanya tathimini hakika taifa
limepiga hatua na hii inajidhihirisha katika katiba inayopendekezwa na
hivyo kuwataka wanawake kuunga mkono katiba hiyo ipite ili kwakua ni
chombo kitakachoweza wanawake kupata haki sawa katika nyanja za siasa na
uongozi.
Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Sofia Simba amesema
miaka 15 tangu ulingo wa Beijin serikali imeweka kipaumbele kwa
kuwezesha wanawake katika sekta mbalimbali zikiwemo nafasi za ajira na
uongozi pamoja na kurekebisha vipengele vinavyokandamizi kwa wanawake
nae mwakilishi wa mataifa amesema maswala ya kijinsia lazima kupewa
kipaumbele kwa taifa lolote ili kuleta maendeleo.
Nao washiriki wa maadhimisho hayo kutoka taasisi mbalimbali za
serikali wamesema maadhimisho hayo yalenge kuwajengea uwezo wanawake
katika fursa za kupata matibabu na ajira zilizo salama.
Katika maadhimisho viongozi na tasisi zilizonyesha mchangano katika
kuendeleza wanawake akiwemo rais Kikwete na Spika wa mbunge la jamhuri
ya muungano na mama Getrude Mongela maadhimisho hayo yamepanbwa na
burudani mbalimbali ikiwemo maandmano na kisha nyimbo zilizotumbuizwa na
wasanii Stara Tomas na Peter Msechu kwa kushirikiana na wafunzi wa
shule ya sekondari ya wasichana Kilakala.