ANGALIA MWANAMKE HUYU ALIYEKAMATWA NA POLISI ALIKOKUWA AMEFICHA DAWA ZA KULEVYA

Kila siku wauzaji wa dawa za kulevya wamekuwa wakibuni njia mpya ya kusafirisha dawa hizo kwa nchi ambazo zimepiga marufuku usafirishaji na utumiaji wa dawa hizo.
Mwanamke mmoja Uingereza amekamatwa baada ya kukutwa akiwa amebeba dawa za kulevya aina ya Cocaine ndani ya sidiria.
26AA9E2500000578-0-image-m-48_1426423833794Mwanamke huyo Nola Williams alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Gatwick, akitokea Jamaica akiwa na mtoto mdogo pamoja na kijana anaejihusisha na biashara hiyo ambaye jina lake ni Raymond Goodison, ambao walikamatwa walipotaka kupanda treni kutoka uwanja wa ndege wa Gatwick kuelekea Victoria ndani ya London.
Wakati  Polisi wakifanya ukaguzi waligundua kilo moja ya cocaine yenye thamani ya dola £180,000 zikiwa imeshonewa kwenye sidiria ya mwanamke huyo.
26AA9ECA00000578-0-image-a-44_1426423257292Nola anasubiri kifungo chake, huku kijana aliyeambatana naye amehukumiwa kifungo cha miaka 13 kwa kosa la kujaribu kuingiza zaidi ya kilo moja ya dawa za kulevya aina ya Cocaine huku ikibainika kuwa sio tukio lake la mara ya kwanza.
nola-mug-shot_3233558b
watuhumiwa wa dawa za kulevya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo