Hii imetokea huko Marekani baada ya mama mmoja kunusurika kifo mara mbili baada ya mtoto wake kumwekea sumu ya kuondoa madoa kwenye kinywaji chake kisa kikiwa ni baada ya kumnyang’anya simu yake aina ya Iphone.
Mtoto huyu mwenye miaka 12 katika jimbo la Colorado Marekani amefunguliwa mashtaka ya kuua na amekiri kuwa alitaka kumuua mama yake ili kulipiza kisasi kwa sababu alichukua simu yake.
Mara ya kwanza mtoto huyo alimwekea mama yake sumu aina ya Chlorine kwenye kinywaji na mama yake hakuweza kubaini ingawa alisema alisikia harufu lakini alihisi glasi aliyotumia haikuoshwa vizuri.
Mama yake aliwaambia maafisa wa polisi kuwa alishangaa aliponusa harufu ya sabuni baada ya kunywa mchanganyiko huo uliotayarishwa na mwanaye huyo.