Malawi ni moja ya nchi ambazo zina
tatizo kubwa la ishu ya ndoa za utotoni, tafiti zinaonyesha karibu nusu
ya wasichana wa nchi hiyo wameolewa wakiwa hawajatimiza miaka 18.
Kutokana na kuendelea kwa tatizo hilo la
ndoa za utotoni, Malawi wamepitisha sheria mpya kuanzia sasa umri
sahihi wa mtoto wa kike kuolewa ni kuanzia miaka 18.
“Sheria hii itasaidia kulinda haki za watoto wetu wa kike.. Hawatakiwi kuozwa wakiwa kwenye umri wa kuwa shule..“– alisema Jessie Kabwila ambaye ni msemaji wa Chama cha Upinzani cha MCP.