HII NI HABARI YA msichana wa kazi ambae aliachiwa mtoto
na bosi wake ambae alikuwa anaumwa lakini hakuwa amezidiwa na baadae
alipigiwa simu na jirani yake na kumueleza kuwa mtoto wake amefariki.
Mama wa mtoto amesema alienda Kariakoo
akamwacha mtoto anacheza, akampa house girl maelekezo ya kumpa maziwa na
dawa, alipofika Kariakoo alimpigia simu na kuulizia hali ya mtoto
akamwambia anacheza na akamsikia kwenye simu.
Muda mfupi baadaye alipigiwa simu na
jirani yake akimwambia kuwa mtoto amezidiwa, mama huyo akamuomba jirani
amsaidie kumpeleka Hospitali, alipopigiwa tena mara ya pili alipewa
taarifa kuwa mtoto amefariki.
Kilichomshangaza ni kuwa baada ya msiba
msichana huyo alimfuata na kumwambia kuwa anamuonea huruma kwani kuna
kitu kilimjia na kumwambia amzidishie mtoto dawa na asimpe chakula kisha
amlaze chini ili kazi yao itimie, mtoto akawa amefariki.
Msichana huyo alipoulizwa alisema kuwa
alimpa mtoto dawa akafariki lakini amekuwa akioteshwa ndoto na ndugu
zake na kuna kitu huwa kinamjia na kumtuma kumdhuru mtoto bila yeye
kujijua, kwa sasa sura ya mtoto inamjia usiku na kumfanya akose
usingizi.