Jeshi la Polisi mkoani Tabora limewakana
askari mgambo walioko stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ambao
wanadaiwa kugeuka kero kwa kamatakamata na kuomba rushwa watu wenye
baiskeli.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda alisema hayo wakati akitoa ufafanuzi wa sakata hilo kwa waandishi wa habari baada ya meneja wa stendi hiyo, Cornery Masawe kutamka askari mgambo hao wamewekwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora Mjini.
Kaganda alisema mgambo hao hawahusiki na ofisi yake wala Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wanawajibika moja kwa moja na halmashauri ya Manispaa Tabora, hivyo aulizwe Mkurugenzi Mtendaji.
Alibainisha kuwa endapo mgambo hao
wangekuwa wameagizwa na ofisi ya OCD, hapo angetoa ufafanuzi wake lakini
hana cha kusema kutokana na mgambo kutowatambua kuwajibika kwake.
Meneja wa stendi ya mabasi yaendayo
mikoani mkoani Tabora, Cornery Masawe kwa mara nyingine alisema mgambo
hao hana majibu lakini akaomba aulizwe Kamanda wa Polisi Wilaya ya
Tabora Mjini, Benjamini Kuzaga.
Kamanda wa Polisi Tabora Mjini,
Benjamini Kuzaga ambaye alipoelezwa juu ya mgambo hao, kwanza alishangaa
na kusema hana majibu na msemaji ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,
Kaganda.
Mgambo pamoja na meneja wa stendi hiyo
wamelalamikiwa na wananchi wakidaiwa wanapokamatwa na baiskeli zao hata
kama hawaendeshi ndani ya stendi hiyo hutozwa faini Sh 20,000, 15,000 au
10,000 lakini