Mzee Abby Sykes ambaye ni Baba mzazi wa
muimbaji wa muziki wa Bongo Fleva Prince Dullysykes,amefariki saa 8
mchana wa leo akiwa hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa ameenda
kwaajili ya kupatiwa matibabu.
Dullysykes ameongea ikiwa
ni pamoja na kuelezea kitu kilichosababisha umauti wa Mzee
Abbysykes>>’Mzee alikua ana vidonda katika miguu ndiyo chanzo
kikubwa,sumu ikasambaa ikasababisha kifo chake,vidonda vilishindwa
kupona kwa ajili ya moshi wa sigara,hakua na tatizo lolote’
‘Mzee vidonda alianza kuugua kwa miezi
4,miezi 2 alikua anavumilia tu lakini miezi 2 ya mwishoni ndiyo ilizidi
kumsumbua,mazishi tunategemea kuyafanya kesho saa 10 kwenye makaburi ya
Kisutu,lakini safari ya kwenda msikitini tutaanza saa 7 mchana.
Bonyeza play kumsikiliza Dullysykes