MKAZI
wa Loksale wilaya ya Monduli, Samwel Petro Shani(47) amelalamikia hatua
ya kuvunjwa mikono yake miwili kwa kipigo cha askari polisi katika
kituo cha Leskale kwa madai ya kushindwa kulipa deni ya shilingi 250,000
alizokuwa akidaiwa ana mfanyabiashara wa eneo hilo.
Aidha
anawatuhumi askari hao kukodiwa na mfanyabiashara mmoja mkazi wa eneo
hilo kwa lengo la kumshikisha adabu baada ya mkazi huyo kushindwa kulipa
deni la sh,250,000 alizokuwa akidaiwa na mfanyabiashara huyo.
Samweli
ameeleza kupokea kipigo hicho ambapo alidai kuwa dhamira ya askari hao
ilikuwa ni kumtoa uhai wake kwani walikuwa wakitumia chuma kinene
kumpiga na kumvunja mikono yake miwili huku mwingine alikuwa
akimshambulia kwa runngu na mateke.
Akizungumza
kwa majonzi,Samweli alieleza kuteswa na askari hao wanaodaiwa kukodiwa
na mfanyabiashara aliyemtaja kwa jina moja la bi Shamimu,ambaye alikuwa
akimdai kiasi hicho cha fedha.
Alieleza
kuwa tukio hilo lilitokea februali 6,mwaka huu majira ya saa 3 usiku na
kwamba aliwatambua askari wawili waliomtesa kwa kipigo kuwa ni Steven
na Justini wote ni askari wa kituo hicho cha Loksale.
''Mnamo
tarehe 6 mwezi huu majira ya saa 3 usiku,walikuja askari wawili wakiwa
wamevaa nguo za kiraia ,walinikuta nimekaa kwenye ukuta nikiwa na kijana
mmoja.Walinikamata na kunifunga pingu wakiwa wamenikandamizia chini
,walinipiga sana na kunivunja mikono yangu miwili'' alisema Samweli
Akisimulia
chanzo cha tukio hilo alisema ,mfanyabishara bi Shamimu alienda katika
kituo hicho cha polisi na kuwaeleza askari hao kuwa alikuwa akinidai
shilingi 250,000 na kwamba sikuwa nimemlipa deni hilo.
''Ni
kweli Shamimu alikuwa akinidai shilingi 250,000 ila nilisha mlipa
shilingi laki moja na kubaki sh,150,000 ,hizo hela kuna msichana
nilimdhamini alikuwa mfanyakazi wa duka lake aliyedai alimwibia ,ndipo
mimi kwa kuwa nilikuwa na mahusiano na msichana huyo nilikubali kulilipa
deni hilo'' alisema Samweli
Alisema
askari hao walimvamia na kumkaba kabali kisha askari mmoja alimfunga
pingu na kuanza kumshambulia kwa kumpiga na rungu na chuma na walipoona
wamepoteza fahamu baada ya kumvunja mikono walimkokota hadi kituo cha
polisi na kuendelea kumpiga sehemu zingine za mwili ikiwemo miguuni.
''Baadae
usiku wakiwa wamenifungia lokapu alikuja mkuu wa kituo na
kuniangalia,alikuta hali yangu ni mbaya na kuondoka bila kusema lolote''
alisema.
Hata
hivyo askari hao waliingiwa na woga kutokana na hali yake na kuamua
kumchukua usiku huo wa manane na kumpeleka katika kituo cha afya kwa
ajili ya matibabu.
Alieleza kuwa kesho yake askari hao walimchukua na kumpeleka kituo cha polisi wilaya ya Monduli na kumweka lokapu.
Aliongeza kuwa mkuu wa upelelezi wa wilaya OC CID,aliyemtaja kwa jina moja la bw Abichi alimfuata akiwa lokapu na kumwambia kuwa anataka ampatie dhamana ila alitakiwa akibaliane na masharti ya dhamana .
Aliongeza kuwa mkuu wa upelelezi wa wilaya OC CID,aliyemtaja kwa jina moja la bw Abichi alimfuata akiwa lokapu na kumwambia kuwa anataka ampatie dhamana ila alitakiwa akibaliane na masharti ya dhamana .
''OC
CID aliniambia kuwa nataka nikupatie dhamana ila kwenye maelezo yako
unatakiwa ueleze kuwa ulikuwa unatoroka ulinzi halali wa polisi ukiwa na
pingu ,na wakati ukikimbia ulianguaka na pingu zikakuvunja mikono yako
''alisema bw Shani.
Aliongeza
kuwa hakukubaliana na kauli hiyo ndipo oc cid alipoamua kumrudisha
lokapu ,ambapo alikaa kwa muda wa siku nne wakimbembeleza akubaliane na
maelezo ya polisi .
Alisema
aliamua kuwa na msimamo huo hadi tarehe 12 walipoamua kumfikisha
mahakama ya wilaya ambapo alisomewa shtaka la kuvunja na kuiba na
kujaribu kutoroka polisi akiwa na pingu ,suala ambalo ni uongo uliolenga
kupoteza haki yake ya kulalamikia jeshi hilo.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa alipotafutwa alikiri kupata malalamiko ya mkazi
huyo ,hata hivyo alieleza kuwa kwa sasa yupo likizo ila aliwasiliana na
mkuu wa kituo cha polisi Monduli(OCD)ili kupata undani wa tukio hilo.
Kwa
upande wa mfanyabiashara ,Shamimu alipotafutwa kupitia simu yake ya
mkononi alikana kukodisha askari wa kumpiga na kumvunja mkono
mlalamikaji ila alieleza kuwa yeye alienda kituoni hapo kupeleka
malalamiko yake ndipo askari hao walipoamua kumfuata mtuhumiwa na kwamba
kilichotokea huko yeye hafahamu.